Somo;
Imani ni kuwa na tarajio la kupata kitu usichokijua au kukiona na kutarajia kukipokea, Ukiwa na imani huwezi kuzuiliwa kuingia mahali popote unapopataka na kuchukua unachokitaka kwa sababu imani uliyonayo inaweza kuingia na kujenga hata mahali pale ambapo watu wengine walishindwa Imani inakua, Ukiwa na imani Roho mtakatifu anakaa ndani yako hivyo lazima imani yako ikue ili uweze kutenda makuu na makubwa ya ajabu(1wakorintho 12:1). Imani ina utofauti wa utendaji kazi kutokana na namna imani yako inavyoamini, Utakapoona utendaji wako wa kiimani uko tofauti na mwingine unatakiwa umuulize Yule anayetoa imani kwamba kwa nini haujafikia kile kiwango cha mafanikio au ufaulu unaoutaka. KUMBUKA,imani inazidishwa ama kuongezwa kwako kutokana na namna ambavyo unaishughulisha imani yako katika kuamini mamo ambayo yanatokea kwako na kufanikiwa kwako kupo katika imani yako. Unaweza ukaamini lakini usiamini katika utendaji wa imani yako, Jambo lolote unalolitaka lipo katika kuamini...