NIMEMUONA YEYE AMBAYE AMENIONA.



NIMEMUONA YEYE AMBAYE AMENIONA.
Tamani kumuona yeye anaekujua wewe tangu siku ya kwanza ya kuumbwa kwako siyo mwanadamu ambae hajui hatma yako, Lipo jambo ambalo unalitaabikia mtafute Yule anaekuona ili akupe haja yako (2Wafalme 19:27-28).
 Usiitumie vibaya neema ya Mungu kwa kufanya dhambi kwa makusudi na kutegemea kwamba utaingia magotini na kuomba rehema Mungu hajaribiwi na unapoamua kumtafuta yeye anaekuona maanisha kumtafuta nae atajidhirihisha kwako usitumie njia ya mkato ili kukidhi hitaji lako kwa maana itakugharimu.
Mtafute yeye naekuona Mungu wetu ni Mungu mwaminifu hakumuumba mwanadamu ili apate taabu, apate shida ila alimuumba kwa kusudi maalum na lazima litimie kwako, Kaa utafakari ni kwa nini unapitia hali uliyonayo sasa usianze kulaumu, na kudhani kwamba Mungu hakuoni, Tamani kumuona yeye anaekuona ili akuvushe kwenye daraja unalopitia usimtazame mwanadamu mtazame Mungu anasema nini juu ya maisha yako.




Maoni