Machapisho

NIMEMUONA YEYE AMBAYE AMENIONA.

Picha
NIMEMUONA YEYE AMBAYE AMENIONA. Tamani kumuona yeye anaekujua wewe tangu siku ya kwanza ya kuumbwa kwako siyo mwanadamu ambae hajui hatma yako, Lipo jambo ambalo unalitaabikia mtafute Yule anaekuona ili akupe haja yako (2Wafalme 19:27-28).   Usiitumie vibaya neema ya Mungu kwa kufanya dhambi kwa makusudi na kutegemea kwamba utaingia magotini na kuomba rehema Mungu hajaribiwi na unapoamua kumtafuta yeye anaekuona maanisha kumtafuta nae atajidhirihisha kwako usitumie njia ya mkato ili kukidhi hitaji lako kwa maana itakugharimu. Mtafute yeye naekuona Mungu wetu ni Mungu mwaminifu hakumuumba mwanadamu ili apate taabu, apate shida ila alimuumba kwa kusudi maalum na lazima litimie kwako, Kaa utafakari ni kwa nini unapitia hali uliyonayo sasa usianze kulaumu, na kudhani kwamba Mungu hakuoni, Tamani kumuona yeye anaekuona ili akuvushe kwenye daraja unalopitia usimtazame mwanadamu mtazame Mungu anasema nini juu ya maisha yako.

ROHO YA IMANI

Picha
ROHO YA IMANI Imani ni kuwa na tarajio la kupata kitu usichokijua au kukiona na kutarajia kukipokea, Ukiwa na imani huwezi kuzuiliwa kuingia mahali popote unapopataka na kuchukua unachokitaka kwa sababu imani uliyonayo inaweza kuingia na kujenga hata mahali pale ambapo watu wengine walishindwa Imani inakua, Ukiwa na imani Roho mtakatifu anakaa ndani yako hivyo lazima imani yako ikue ili uweze kutenda makuu na makubwa ya ajabu(1wakorintho 12:1) Imani ina utofauti wa utendaji kazi kutokana na namna imani yako inavyoamini, Utakapoona utendaji wako wa kiimani uko tofauti na mwingine unatakiwa umuulize Yule anayetoa imani kwamba kwa nini haujafikia kile kiwango cha mafanikio au ufaulu unaoutaka KUMBUKA,imani inazidishwa ama kuongezwa kwako kutokana na namna ambavyo unaishughulisha imani yako katika kuamini mamo ambayo yanatokea kwako na kufanikiwa kwako kupo katika imani yako Unaweza ukaamini lakini usiamini katika utendaji wa imani yako, Jambo lolote unalolitaka lipo ka...

Somo;

Picha
Imani ni kuwa na tarajio la kupata kitu usichokijua au kukiona na kutarajia kukipokea, Ukiwa na imani huwezi kuzuiliwa kuingia mahali popote unapopataka na kuchukua unachokitaka kwa sababu imani uliyonayo inaweza kuingia na kujenga hata mahali pale ambapo watu wengine walishindwa Imani inakua, Ukiwa na imani Roho mtakatifu anakaa ndani yako hivyo lazima imani yako ikue ili uweze kutenda makuu na makubwa ya ajabu(1wakorintho 12:1). Imani ina utofauti wa utendaji kazi kutokana na namna imani yako inavyoamini, Utakapoona utendaji wako wa kiimani uko tofauti na mwingine unatakiwa umuulize Yule anayetoa imani kwamba kwa nini haujafikia kile kiwango cha mafanikio au ufaulu unaoutaka. KUMBUKA,imani inazidishwa ama kuongezwa kwako kutokana na namna ambavyo unaishughulisha imani yako katika kuamini mamo ambayo yanatokea kwako na kufanikiwa kwako kupo katika imani yako. Unaweza ukaamini lakini usiamini katika utendaji wa imani yako, Jambo lolote unalolitaka lipo katika kuamini...