ROHO YA IMANI
ROHO YA IMANI
Imani ni kuwa
na tarajio la kupata kitu usichokijua au kukiona na kutarajia kukipokea, Ukiwa
na imani huwezi kuzuiliwa kuingia mahali popote unapopataka na kuchukua
unachokitaka kwa sababu imani uliyonayo inaweza kuingia na kujenga hata mahali
pale ambapo watu wengine walishindwa
Imani inakua,
Ukiwa na imani Roho mtakatifu anakaa ndani yako hivyo lazima imani yako ikue
ili uweze kutenda makuu na makubwa ya ajabu(1wakorintho 12:1)
Imani ina
utofauti wa utendaji kazi kutokana na namna imani yako inavyoamini, Utakapoona
utendaji wako wa kiimani uko tofauti na mwingine unatakiwa umuulize Yule
anayetoa imani kwamba kwa nini haujafikia kile kiwango cha mafanikio au ufaulu
unaoutaka
KUMBUKA,imani
inazidishwa ama kuongezwa kwako kutokana na namna ambavyo unaishughulisha imani
yako katika kuamini mamo ambayo yanatokea kwako na kufanikiwa kwako kupo katika
imani yako
Unaweza
ukaamini lakini usiamini katika utendaji wa imani yako, Jambo lolote
unalolitaka lipo katika kuamini(Warumi 17)


Maoni
Chapisha Maoni